Burudani

Video ya Gangnam Style yavunja kiwango cha mwisho cha views za YouTube!

Video ya muziki ya msanii wa Korea Kusini, Psy, ‘Gangnam Style’, imepitiliza kiwango cha mwisho cha views za Youtube na hivyo kuufanya mtandao huo uongezee kaunta yake.

YouTube imedai kuwa, video imeangaliwa zaidi kuliko zote duniani na hadi sasa imeangaliwa kwa zaidi ya mara 2,155,016,530. Na sasa Youtube imebadilisha kiwango chake cha juu kuwa 9,223,372,036,854,775,808, au zaidi ya quintillion 9.

Unaitamkaje 9,223,372,036,854,775,808? Quintillion tisa, quadrillion mia mbili na ishirini na tatu, trillion mia tatu na sabini na mbili, bilioni thelathini na sita, milioni mia nane na hamsini na nne, laki saba na elfu sabini na tano, mia nane na nane.

Awali kiwango cha mwisho cha Youtube kilikuwa ni 2,147,483,647.

December 1, Youtube iliandika:

“We never thought a video would be watched in numbers greater than a 32-bit integer… but that was before we met Psy.”

Na sasa inatumia 64-bit integer kwenye kaunta yake na hiyo ina maana kuwa video zinaweza kuangaliwa hadi kwa 9.22 quintillion.

Video ya pili iliongaliwa zaidi kwenye mtandao huo ni Baby ya Justin Bieber ambayo hata hivyo ipo nyuma kwa zaidi ya views bilioni moja kwa Gangnam Style.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents