Burudani

Video ya wimbo ‘Saka Hela’ ni ya gharama kubwa, nimeifanya ili kuonyesha naweza – Nay

Rapper Nay wa Mitego Jumatatu hii ameachia video yake mpya ya wimbo ‘Saka Hela’. Video hiyo imeonyesha kupokewa kwa shangwe ya mashabiki wa muziki.
Nay akiwa kwenye maandalizi ya kazi mpya

Akizungumza na Bongo5 Jumanne hii, Nay wa Mitego amesema baada ya video hiyo kuonekana katika runinga pamoja na mtandao wa Youtube kwa mara ya kwanza amepokea simu nyingi kuhusu kazi hiyo.

“Kwa mapokezi haya namshukuru mungu, hii ni video ya pesa nyingi na watu wameipokea vizuri sana kusema kwali, yaani ndani ya masaa machache baada ya kuiachia tu nimeshaona nini nimekifanya kwenye ile kazi,” alisema Nay.

“Lakini yote haya yametokana na kazi nzuri, nimehakikisha nimetumia pesa nyingi sana, ukiangalia magari, helikopta, sikutaka isimame tu, inatembea ili kuonyesha uhalisia wa kila kitu. Kwa hiyo ni video fulani ambayo nilikuwa nataka kuonyesha kuwa naweza pia kufanya vitu vikubwa,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents