Bongo Movie

Wabunge wakosoa marekebisho kwenye sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza (1976)

Wabunge mbalimbali wakiwemo John Mnyika, Tundu Lissu na Halima Mdee, leo wamekosoa marekebisho kwenye sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza (1976) ambayo ni sehemu ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba 3 wa Mwaka 2013,uliowasilishwa bungeni leo.

26

Katika marekebisho hayo, filamu itakayokuwa na lugha chafu itakabiliwa na adhabu ya kulipa faini ya shilingi milioni tano kutoka ile ya awali ya Sh 15,000 au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela badala ya mwaka mmoja wa awali.

Muswada huo umewasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

“Kama kungekuwa na tatizo kwenye sheria hii kama ilivyo, mwanasheria mkuu wa serikali angetoa mfano mmoja wa mtu aliyepatikana na hatia chini ya sheria tangu mwaka 1976 ilipotungwa, akatozwa faini, ikaonekana ndogo, akarudia kosa. Hawezi kusema hivyo sababu hawajawahi kushitaki mtu hata mmoja,” alisema Tundu Lissu.

“Sababu yenyewe ya sheria kuwepo actually is questionable. Unaletaje muswada unaosema tuongezee adhabu ya sheria hii mara 600 na kwa asilimia laki 3? Youu cannot be serious. Hivi hamjawahi kusikia Hollywood, hamjawahi kusikia Bollywood, hamjawahi kusikia Nollywood? Watu wanatengeneza billions of dollars out of film industry sisi tunasema tufunge watu.”

Naye mbunge wa Kawe, Halima Mdee alisema pendekezo la kuweka faini ya shilingi milioni tano lifutwe na kuwa shilingi laki 5 na kudai kuwa serikali haijatengeneza mazingira yoyote ya kulinda kazi za wasanii wa Tanzania.

“Badala ya kuhakikisha kwamba, vyombo vyake ambavyo vinaundwa kisheria vitekeleze wajibu wake wa kukagua hizi kazi zinazotolewa, ambazo zinatolewa kwa vijana wetu kuhangaika wenyewe pasipo msaada wowote wa serikali, kitu pekee inachofikiria ni kuongeza faini,” alisema Mdee.

“Tujengee mazingira vijana wetu kwanza ndipo tutoze faini nzito,”aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents