Michezo

Waziri Mwakyembe akabidhi bendera kwa Serengeti Boys

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) tarehe 3 Aprili 2017 ameshiriki kwenye zoezi la kuwaaga na kuwapatia bendera ya Taifa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).

Mhe. Mwakyembe amewaasa vijana wa Serengeti kuliwakilisha vyema Taifa kwenye michuano ya AFCON wanayotarajia kwenda kushiriki hivi karibuni.

Mhe. Mwakyembe akiongozana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi aliwahakikishia vijana wa Serengeti utayari wa Serikali katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Vilevile, Mhe. Mwakyembe ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuwachangia Serengeti Boys ili waweze kuwa na ushiriki bora katika michezo ya maandalizi nchini Morroco na Cameroun na baadaye katika michuano ya AFCON, nchini Gabon.

Sambamba na hilo Mhe. Mwakyembe aliwaongoza wananchi waliofika uwanja wa Taifa kuishangilia Serengeti boys iliyokuwa ikicheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya vijana kutoka Ghana, ambapo Serengeti boys wameweza kurudisha magoli mawili na matokeo hadi mwisho yakawa sare ya 2-2.

“Mpira umemalizika tumetoka sare ya 2-2. Mechi ilikuwa ngumu na ni zoezi zuri kwa Serengeti Boys. Tuzidi kuwatia hamasa,” amesema Malinzi mara baada ya mchezo huo jana jioni.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents