Burudani

Weusi waingia studio na Navio wa Uganda kufanya ‘Gere’ East African remix waliyowashirikisha Naziz na Collo

Kundi la Weusi limemeingia tena studio, lakini safari hii wakiwa na rapper Navio kutoka Uganda ambaye yupo jijini Dar es salaam kwa sasa.

Weusi and Navio

Weusi wamemuongeza Navio kwenye remix ya single yao ‘Gere’, ambayo tayari walitangaza kuwa wameifanyia remix nchini Kenya miezi kadhaa iliyopita na kuwashirikisha Collo na Naziz na hivyo kuifanya kuwa ni remix iliyohusisha wasanii wa nchi tatu za Africa mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda.

Joh alishare picha Instagram akiwa studio na Navio, Nahreel, Lordize na G-Nako na kuandika:

“Studioni saa hii with @naviomusic @gnakowarawara @nahreel #Lordize #Gere Eastafrican remix feat.#collo #naziz” aliandika Joh Makini Instagram.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents