Technology

Yaelezwa magari mapya yanayotumia umeme, kuwekwa chombo maalumu cha kupiga kelele kwa ajili ya usalama kwa watembea kwa miguu, fahamu zaidi

Yaelezwa magari mapya yanayotumia umeme, kuwekwa chombo maalumu cha kupiga kelele kwa ajili ya usalama kwa watembea kwa miguu, fahamu zaidi

Magari mapya yanayotumia umeme yanapaswa kuwekwa chombo kitakachotoa kelele, hii ni chini ya sheria mpya ya EU ambayo inaanza kutekelezwa Jumatatu.

Hatua hii mpya imekuja kutokana na madai kuwa magari ya umeme hayana sauti na kuwafanya watu ambao hawatumii magari wakiwa barabarani kuwa hataranini kwa kuwa magari hayo hayasikiki mlio wake yakiwa karibu.

Kwa mujibu wa BBC. Aina zote mpya za magari aina ya Four-wheel yanapaswa kufungwa chombo hicho ambacho kitakuwa kikitoa mlio kama wa injini. Kifaa hicho kiitwacho acoustic vehicle alert system (Avas) lazima kitoe mlio wakati gari inarudi nyuma au kusafiri kwa umbali wa kilometa 19 kwa saa

Umoja wa Ulaya unasema magari yanapaswa kuwa na kelele yakiwa karibu na watembea kwa miguu yanapokuwa yakitembea taratibu, ingawa madereva watakuwa na uwezo wa kukizima kifaa hicho kama wanafikiri kuna ulazima.

Taasisi zinazosimamia mbwa wanaotoa usaidizi kwa watu wenye uhitaji barabarani kama vile wale wasioona na walemavu wa viungo wamesema kuwa ni vigumu kubaini kama magari yasiyo na sauti yako karibu, na wameunga mkono mabadiliko haya, lakini wanasema kuwa vyombo vya moto vinavyotumia umeme vinapaswa kutoa sauti vikiwa kwenye mwendo wowote.

Waziri wa barabara Michael Ellis amesema serikali ilitaka ”faida ya usafiri wa kutunza mazingira kumfikia kila mmoja” na ameeleza kuelewa maoni ya wale wenye ulemavu wa kutoona.

”Matakwa mapya yatawafanya watu wanaotembea kwa miguu kuwa na hali ya kujiamini wakiwa wanavuka barabara,” aliongeza.

Ifikikapo mwaka 2021 magari yote ya umeme yanapaswa kuwa na kifaa cha AVAS, si kwa magari mapya pekee.

Serikali ilitangaza mipango ya kupiga marufuku magari yanayotumia mafuta ya petroli na Dizeli kuuzwa mwaka 2040.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents