Michezo

Bruce Arena amrithi Jurgen Klinsmann Marekani

Baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Marekani, Jurgen Klinsmann nafasi yake imechukuliwa na kocha Bruce Arena anateuliwa kuwa meneja mkuu kwa mara ya pili.

bruce-arena-la-galaxy
Bruce Arena ambaye ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya taifa ya Marekani

Mmarekani huyo amabaye ana umri wa miaka 65, ataiyaga timu yake ya LA Galaxy, ilikuchukua nafasi hiyo, aliongoza nchi yake mwaka 2002 hatua ya robo fainali alipoanza kuhudumu kwa mara ya kwanza.

Bruce Arena ameshinda vikombe vitano katika ligi ya MSL akiiongoza timu ya LA Galaxy ya jiji la New York na DC United.

Marekani saivi wamo katika nafasi ya mwisho ya nchi sita zinazoshindania kufuzu Kombe la Dunia kutoka bara la Amerika, nyuma ya mataifa madogo kama vile Panama na Honduras.

“Ukipata nafasi ya kuwa meneja wa timu ya taifa ,ni heshima,” Arena amesema.

Ninauhakika tutachukua hatua zifaazo na kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazoandaliwa Urusi mwaka 2018.

Arena ataanza kazi kama kocha tarehe 1 mwezi Disemba,na mechi yake ya kwanza itakuwa nyumbani dhidi ya Honduras tarehe 24 mechi mwaka 2017

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents