Michezo

Fernandinho asaini mkataba mpya Man City

Kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Brazili, Fernandinho Luiz Roza ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia klabu ya Manchester City utakao muweka Etihad mpaka mwaka 2020.

Fernandinho mwenye umri wa miaka 32, ameiyambia tovuti ya klabu hiyo kuwa “Hii ni klabu ambayo inamipango bora zaidi ya baadae na mimi nahitaji kuwa sehemu ya mikakati hiyo.”

Fernandinho ameongeza “Ikiwa chini ya Pep nafikiria kuwa tutashinda mataji na tutafanya mambo muhimu na makubwa tukicheza mpira wenye mvuto na wakushambulia.”

Fernandinho Roza  ametua Man City mwaka 2013 akitokea Shakhtar Donetsk kwa usajili wa miaka sita.

Akifanikiwa kucheza michezo 46 ndani ya City na kushinda taji la Premier League na League Cup katika msimu wake wa kwanza ndani ya klabu.

Baada ya hapo akafanikiwa tena kuisaidia timu yake kunyakuwa taji la League Cup kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya Liverpool katika dimba la Wembley mwaka 2016 na kuiwezesha kutinga nusu fainali ya michuano ya Champions League. Kwa jumla amecheza mara 212 na Blues na kufunga mabao 19.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents