Jinsi tunavyojitolea kuziandaa klabu zetu kubwa tufanye hivyo kwa Taifa Stars – Kocha (+Video)

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Etienne Ndayiragije amekipongeza kikosi chake kwa kujituma na kujitolea mpaka kufanikiwa kuondoka na alama moja mbele ya Tunisia huku akisisitiza umuhimu wa kuwa na muda wa kutosha wa kufanya maandalizi na kutolea mfano klabu kubwa nchini zinavyojitolea katika kujiandaa basi nguvu hiyo ihamishiwe na katika timu ya Taifa.

”Chakwanza nawapongeza wamejaribu kutoa kile ambacho wanacho, nikiangalia kile nilichowekeza nikiangalia na walichotoa nawapongeza kwa hilo, Naamini kuwa kila kitu kwenye soka kinaandaliwa kwa hiyo maandalizi, kwa hiyo maandalizi yetu yaliishia hapa, tukihitaji kwenda mbele tuongeze maandalizi.”- Ndayiragije

Etienne Ndayiragije amesisitiza jinsi zinavyojitolea katika kufanya maandalizi klabu kubwa nchini nguvu hizo hizo zingetumika kuiyandaa timu ya taifa anaimani vipaji vipo na uwezo upo ”Jinsi tunajitolea kuandaa hizi klabu zetu nyingine kuu, tungeongeza tena kwa kuandaa timu yetu ya taifa nina imani kuwa vipaji vipo na uwezo upo .”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW