Tupo Nawe

Klopp akunwa na Alisson Becker ‘Ningemlipa mara mbili kama ningefahamu uwezo wake toka mapema’

Meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amempongeza mlindalango wake, Alisson Becker kwa kazi nzuri aliyoifanya hapo jana usiku kwenye mechi yao dhidi ya Napoli na kupelekea kufuzu hatua ya 16 bora ya Champions League.

Becker raia wa Brazili amesainiwa kwa dau la pauni milioni 67, hapo jana aliiopoa michomo ya straika wa Napoli na timu ya taifa ya Poland, Arkadiusz Milik akitoka kwenye majeraha.

Akizungumzia ubora wa kipa wake aliyouonyesha hapo jana Klopp ameiyambia Viasport kuwa “Mlindalango wetu ametuokoa msimu huu, sikufahamu amewezaje kuokoa. Tunashukuru Mungu kwakuwa  na yeye laiti kama ningefahamu ubora wake toka awali ningelimlipa marambili, nafikiri hakuna mtu yoyote aliyetarajia kama angeweza kuokoa katika mazingira yale.”

“Alikuwa na vitu vingi vya kufanya, lakini alitulia ila bado anahitaji vijana wakumzunguka, huwezi kuamini kile ambacho vijana wamefanya usiku wa jana.”

Liverpool ishukuru pia kupata bao katika kipindi cha kwanza kutoka kwa Mohamed Salah, lililowasaidia kushika nafasi ya pili kwenye Group C nyuma ya Paris Saint-Germain.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW