Tupo Nawe

Madrid wapo radhi kumtoa sadaka mchezaji huyu kumpata Pogba, Herrera ‘maisha ya soka ya United yalikuwa magumu’

Real Madrid watakuwa tayari kutoa ofa ya kiungo wa Colombia James Rodriguez, 28, kubadilishana na kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa na Manchester United Paul Pogba,26. (El Desmarque, via Metro)

Man Utd

Kiungo wa Paris St-Germainm Ander Herrera, 30, amesema alifikiri mpira wa miguu haukuwa na umuhimu tena wakati alipokuwa Manchester United, kutokana na mfumo mgumu wa timu hiyo (Metro)

Inter Milan wanamtolea macho mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud. (Gazzetta dello Sport – via Sun)

Mshambuliaji wa Ajax Quincy Promes, 27, amesema yuko tayari kwa uhamisho kuelekea ligi ya Primia siku za usoni,kauli hiyo ameitoa wakati ambapo Arsenal na Liverpool wakiwa na nia ya kumnyakua mchezaji huyo. (Mail)

Kocha wa timu ya taifa Uingereza Gareth Southgate amesema vikwazo vinavyotolewa kutokana na vitendo vya ubaguzi wa rangi vinapaswa kuwa vikali. (Express)

Manchester United itaweka mezani pauni milioni 42 kwa ajili ya kiungo wa Tottenham na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen, 27, ifikapo mwezi Januari.(El Desmarque – via Express)Cedric SoaresMchezaji wa nafasi ya ulinzi klabu ya Southampton, Cedric Soares

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema mchezaji wa nafasi ya ulinzi ya Argentina Marcos Rojo anajiandaa kuendelea kubaki na klabu hiyo. Mchezaji huyo, 29 alifanya mazungumzo na Everton kuhusu uhamisho. (Manchester Evening News)

Kocha wa Southampton Ralph Hasenhuttl amesisitiza kuwa hana tatizo na kumchezesha mchezaji wa nafasi ya ulinzi Cedric Soares, 28, au kiungo Pierre-Emile Hojbjerg, 24, pamoja na ukweli kuwa mikataba yao inaelekea ukingoni.(Southern Daily Echo

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW