Mfahamu mrithi wa Pochettino ndani ya Tottenham kama kocha huyo atajiunga na Manchester United
Inaelezwa kuwa endapo klabu ya Tottenham itaondokewa na kocha wake, Mauricio Pochettino kuhamia Manchester United basi Eddie Howe anatarajiwa kurithi mikoba yake.
Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino
Spurs inakabiliwa na vita ya kupigania kubaki kwa meneja wake dhidi ya Manchester United ambayo inaelezwa kumhitaji kwaajili ya kuziba pengo la Jose Mourinho huku Real madrid ikionekana kumnyemelea.
Kocha wa Bournemouth, Eddie Howe
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy itapata faida ya pauni milioni 40 ili kumuwachia, Muargentine, Pochettino ambaye ameonyesha kusisitiza kuondoka huku ikisemekana kutua United au Real.
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham, Daniel Levy
Real na United zipotayari kuboresha mshahara anaopokea sasa Pochettino wa pauni milioni, 8.5 kwa msimu huku ikiwagharimu pauni milioni 34 kwaajili ya kuvunja mkataba wake na Spurs .
United ipotayari kumfanya Pochettino kuwa ndiyochaguo lao namba moja kuwa mbadala wa Jose Mourinho ambaye ametimuliwa kazi siku ya Jumanne.
Tottenham wameonyesha utayari wao wa kwa lolote ambalo linaweza kutokea kwa na kuonekana kujiandaa kumchukua, Howe kutoka Bournemouth.