Burudani

Mshenga wa Nuh Mziwanda kufanikisha ndoa ya msanii mwingine

Aliyekuwa mshenga wa Nuh Mziwanda, meneja HK amewaka wazi kuwa yupo mbioni kufanikisha ndoa ya msanii Dulla Makabila na muigizaji wa filamu Husna Sajent.

Dulla Makabila na Husna Sajent

HK alifanikisha kufungwa ndoa kati ya Nuh Mziwanda na Nawal ambao wameachana hivi karibuni, hata hivyo amedai kuwa ndoa ya Dulla na Husna itadumu.

“Hii itakaa kwa muda mrefu kwanza wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano na ninaamini wanapoelekea wanaelekea sehemu ambayo haitakaa kuwaangusha. Kuna vitu vingine vinaenda chini kwa chini lakini vikija kufumuka wewe unaona kama vipya,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Hawezi kunitia aibu vijana wangu nawakubali, ni vijana ambao nawakubali kwa dhati, wanapokuwa na tatizo lao kimapenzi wakilifikisha kwangu nawatatulia kabisa na ninapowatatulia wenyewe wanahisi kabisa huyo ndio msaada wangu,” amesisitiza.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents