Michezo

Pierre Lechantre rasmi kocha mpya Simba SC (+picha)

Klabu ya Simba hii leo imemtambulisha rasmi kacha wake raia wa Ufaransa, Pierre Lechantre na kuchukua mikoba ya Joseph Omog aliyetimuliwa kazi mwishoni mwa mwaka jana  na sasa ataanza kazi baada ya mchezo na Kagera Sugar.

Kocha Lichantre ameshawahi kufundisha vilabu kadhaa duniani kikiwemo kikosi cha Timu ya Taifa ya Cameroon kilichotwaa ubingwa wa Africa 2000.

Lechantre pia alipata kuwa kocha bora wa Afrika mwaka 2001 na barani Asia mwaka 2012.

Pierre Lechantre sasa ataungana na kocha msaidizi Masoud Juma, Mtunisia Aymen Mohammed Habib katika kazi ya kukifundisha kikosi cha Simba SC ambacho kwa sasa kinaongoza ligi kwa kuwa na jumla ya pointi 29.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents