Michezo

Usajili wa simba kufuru, Deogratius Munish ‘Dida’ ndani na wengine hawa hapa

Klabu ya Simba imewatambulisha rasmi wachezaji wake wapya watatu akiwemo aliyekuwa Mlinda Mlango wa Yanga, Deogratius Munish ‘Dida’ kwaajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kombe la Kagame.

Wachezaji wengine waliyotambulishwa hii leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo iliyopo jijini Dar es salaam ni pamoja na beki Pascal Wawa aliyewahi kuitumikia Azam FC na Meddie Kagere kutoka Gor Mahia FC ya Kenya.

Mlinda Mlango Deogratius Munish amekabidhiwa jezi na 32, Kagere 14 na Pascal Wawa  27 huku afisa habari wa Simba , Haji Manara akisema kuwa usajili huo umelenga kuimarisha kikosi chao ambacho kinakabiliwa na michuano ya kitaifa na kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents