Burudani
Manny Pacquiao ni mmoja wa majaji kwenye Miss Universe 2014
Bondia maarufu wa nchini Ufilipino, Manny Pacquiao ni mmoja wa majaji kwenye shindano la Miss Universe 2014.
Shindano hilo litafanyika Jan. 25 nchini Marekani ambapo Miss Universe 2013, Gabriela Isler wa Venezuela atamvisha taji Miss Universe 2014.
Majaji wengeni ni pamoja na muigizaji maarufu wa tamthilia za kilatin, William Levy, ,Louis Roe, staa wa The Real Housewives of Beverly Hills, Lisa Vanderpump na Kristin Cavallari.
Miss Universe Tanzania, Nale Boniface
Tanzania inawakilishwa na Nale Boniface. Jumla ya washiriki 88 wanawania taji hilo.