Jay Z na Will Smith waungana kutayarisha series ya HBO
Jay Z na Will Smith wataungana kama watayarishaji wa series itakayorushwa kwenye kituo cha runinga cha HBO.
Kwa mujibu wa Entertainment Weekly, Jay Z na Will Smith wametajwa pamoja na Jay Brown, James Lassiter na Aaron Kaplan kuwa watayarishaji wa miniseries kumhusu Emmett Till.
Mwaka 1955, kijana wa miaka 14 mmarekani mweusi Till aliuawa kikatili na Roy Bryant na J.W. Mlam kwa kuongea na msichana wa kizungu mwenye miaka 21, Carolyn Bryant.
Till alipigwa bila huruma kabla ya kupigwa risasi kichwani na mwili wake kutupwa kwenye mto wa Tallahatchie. Bryant na Milam waliachiwa huru baada ya kudaiwa hawakuwa na hatia za mauaji ya Till.
Miezi michache baadaye, wawili hao walifanya mahojiano na jarida la Look na kukiri kuwa walimuua mtoto huyo. Hata hivyo Bryant na Milam hawakuhumiwa tena kwa mauaji ya Till.
Will Smith na Jay Z wana historia ya kufanya kazi pamoja kwakuwa walitengeneza filamu ya Annie, iliyochezwa na Jamie Foxx.
Utengenezaji wa filamu hiyo bado upo kwenye hatua za awali sana na Roc Nation, Overbrook na Kapital Entertainment ni makampuni ya utayarishaji yatakayohusika.