Diamond Platnumz

Diamond na Wema Sepetu kwenda Malindi, Kenya kupiga show


Couple maarufu nchini Tanzania inayofananishwa na ile iliyovunjika na inayotaka kurejea ya Chris Brown na Rihanna, ya Diamond na Wema Sepetu, inatarajiwa kumake headline mjini Malindi, Kenya hivi karibuni.

Kwa mujibu wa gazeti la The Star la Kenya, Diamond ambaye jina lake halisi ni Abdul Naseeb, ataongozana na mwandani wake Wema Sepetu kwenye show itakayofanyika Club Pata Pata mjini Malindi.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa hitmaker huyo wa Mawazo, mjini Malindi.
Taarifa hizo zimetolewa na mkurugenzi wa klabu hiyo Fedele Grasi.

Tarehe 1 mwezi huu Diamond alipiga show ya nguvu mjini Washington DC, Marekani japo hakuongozana na Wema ambaye alikuwa kwenye tour ya Fiesta na wasanii wengine wa Bongo movies.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents