Michezo

Haya ndio walioshinda tuzo za mwezi August ligi kuu Uingereza

Haya ndio walioshinda tuzo za mwezi August ligi kuu Uingereza

Katika tuzo ambazo zinatolewa kila mwezi katika ligi kuu nchini Uingereza za mchezaji bora wa mwezi,goli bora la mwezi na kocha bora wa mwezi,tayari zimeshatangazwa na chama cha soka nchini humo FA.

Katika tuzo zilizotoka msimu uliopita tulimuona mfungaji bora wa ligi hiyo msimu uliopita mchezaji wa Liverpool na taifa la Misri Mohamed Salah,aliweza kushinda tuzo za mchezaji bora wa mwezi alishinda mara tano lakini awamu hii mchezaji huyo hajafakiwa kupata tuzo hata moja.

Mapema leo chama hicho cha soka nchini humo limewatangaza wachezaji wafuatao kushinda tuzo hiyo:-Mchezaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza mwezi huu August ameweza kushinda Mbrazil wa kwanza kuweza kushinda tuzo hiyo pia mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs Lucas Moura,ambaye alifanikiwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Spurs kufunga magoli mawili katika uwanja wa Old Trafford.

Pia mchezaji aliyefunga goli bora la mwezi ni mchezaji wa klabu ya Fulham Jean Michaël Seri raia wa Ivory Cost ambaye goli lake alifunga dhidi ya Burley.

Katika kipengele cha Meneja bora wa mwezi amefanikiwa kushinda kocha wa klabu ya Watford Javie Gracia raia wa Uhispania kwani ameisaidia klabu yake ya Watford kuanikiwa kushinda michezo yake yote minne na kuwa miongoni mwa timu zenye alama nyingi,ikiwa na alama 12 ikiungana na vinara Liverpool pamoja na Chelsea zote zikiwa na alama 12.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents