Habari

Kenya, Somalia zasubiri uamuzi wa mahakama mzozo wa mpaka

Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), yenye makao yake mjini Hague nchini Uholanzi, inatarajiwa kutoa hukumu yake leo siku ya Jumanne kuhusu kesi ya mpaka wa maji kwenye Bahari Hindi kati ya Kenya na Somalia.

Uamuzi wa Mahakama hiyo unatarajiwa kutolewa baada ya Kenya wiki iliyopita, kusema kuwa haitatambua uamuzi wa Mahakama hiyo, lakini pia haitambui Mahakama hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Kesi hiyo iliwasilishwa na Somalia  mwaka 2014 ikidai kuwa jirani yake Kenya ilikuwa imechukua sehemu ya bahari yake, suala ambalo limesababisha mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Somalia inataka mpaka huo wa majini kuchorwa upya, kwa kufuata mpaka ya ardhini huku Kenya ikidai kuwa tangu mwanzo imekuwa ikichukua mkondo wa mstari wa usawa,

Mwezi Machi, Kenya ilijiondoa kwenye kesi hiyo, kwa kile ilichoeleza kuwa, Mahakama hiyo ilikuwa na upendeleo kuhusu eneo hilo lenye mzozo, ukubwa wa Kilomita 160,000 katika bahari ya Hindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents