Burudani
Jon Myuziki akamilisha wimbo wa Acha Kulia
Miongoni mwanamuziki aliyekuwa muasisi wa bendi ya Machozi, akiwa na mwanadada Lady Jay Dee, Jon Myuziki amesema kwa sasa amekamilisha wimbo wake wa Acha Kulia ili kuwatia moyo Wanzania ambao wamekuwa wakiingia kwenye matatizo.
Jon hivi sasa anasema amezindua bendi yake ya The Sweet Band, yenye nyimbo ya Sambona ambayo inapiga nyimbo za kiasili, na mchanganyiko. anasema hata hivyo anatarajia kufanya mengi katika bendi hiyo, kwakuwa amejipanga kwaajili ya kufanya kazi ya muziki.