Burudani

Linex: Mimi sijawahi kuwa mvuta bangi maisha yangu yote na kama ninavuta Mungu ananiona

Kuna baadhi ya watu ambao huamini kuwa mtu akishakuwa msanii wa muziki ni lazima atakua mtumiaji wa vilevi kama bangi, na wapo wanaoamini kuwa binti akishaingia kwenye sanaa ya urembo pia ni lazima atajihusisha na umalaya, kitu ambacho si kweli kwasababu hiyo ni tabia ya mtu binafsi.

Linex

Linex Sunday Mjeda leo ameamua kujibu swali ambalo amekuwa akikutana nalo kila mara katika mahojiano, la kama anavuta bangi ama laa kwasababu ya muonekano wake na pia kuwa msanii.

Kupitia Facebook Linex ameandika:

“Kwa mala ya kwanza Leo nimegoma kujibu swali ambalo nimekua nikiulizwa Sana na vyombo vya habari na swali lenyewe ni kuhusu mimi kujihusisha na matumizi ya uvutaji Bangi. Leo nawambia watanzania na wasio watanzania Mimi sijawahi kua mvuta Bangi maisha yangu yote na Kama nna vuta Mungu ananiona na ningekua mvuta bangi nisingekua na sababu ya kukataa.

Wavuta bangi hamuwasemi hamuwaulizi swali hilo Mimi nisievuta ndo kila siku naulizwa hlo swali narudia tena Sijawahi kua mvuta Bangi sina ratiba ya kutumia dawa za aina yoyote ya kulevya Msinijudge kwa muonekano wangu hivi ndivyo nilivyo na siwezi kua MTU mwingine ‪#‎Sunday‬ Mangu”.

linex kuhusu bangi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents