Benki ya Exim yaandaa iftar kwa wadau wake wote
Benki ya Exim imeandaafutari ya pamoja kwa wateja wake katika hafla iliyofanyikakatika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam mnamo tarehe15 mwezi Machi 2024.
Mgeni Rasmi katika tukio hili alikuwa Sheikh Mkuu waMkoa Dar es Salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, akiwakilisha waumini wa dini ya Kiislam ambao wapokwenye mfungo katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani.
Akizungumza katika hafla hiyo, Sheikh mkuu wa mkoa waDar es salaam, Sheikh Walid Alhad Omar, aliipongeza Benkiya Exim kwa juhudi zake katika kukuza maendeleo yakijamii na kueleza shukrani zake kwa mchango wa benkihiyo kwa jamii. Alisema, “Benki ya Exim inaonyeshadhamira ya kweli katika kutumikia wateja wake na jamiikwa ujumla, lengo kuu la Ramadhani ni kuleta watu pamoja, na usiku huu, benki ya Exim imehakikisha kuendeleza lengohilo kwa vitendo”.
Bwana Jaffari Matundu, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki yaExim, aliwakaribisha wadau wote katika Iftar hiyo hukuakitambua mahusiano mazuri ya tija yaliopo baina ya Benkiya Exim na wateja wake na umuhimu wa kuyaendeleza kwaajli ya ustawi na maendeleo ya jamii.
“Wateja wetu ni zaidi ya wateja tu, ni sehemu muhimu ya familia yetu. Tunaona kila mmoja wenu kama mshirika namwenzetu katika safari yetu ya mafanikio”, alisisitiza JaffariMatundu.
Pia, Mkurugenzi huyo alizungumzia hatua na maboreshombalimbali ambayo yamefanywa na benki ya Exim ilikuendana na mabadiliko katika sekta mbalimbali ikiwemomaendeleo ya teknolojia ya kidijitali na kusogeza hudumakwa wateja.
Jaffari alifafanua kuwa, “tumefanya maboresho makubwa katika mfumo wetu wa Benki ili kuendelea kuhudumia wateja wetu vizuri zaidi kwa kutoa huduma zinazoendana na mabadiliko ya kidigitali”.
“Vile vile tumeendelea kuongeza idadi ya Mawakala wetu (maarufu kama Exim Wakala) ili kuleta huduma zetu karibuna wateja wetu popote walipo”, alimalizia Afisa MtendajiMkuu huyo.
Exim Bank pia imeboresha huduma za kidijitali kwa watejawake ambapo wanaweza kupata huduma za kibenki popotepale walipo ndani na nje ya Tanzania. Hii ni kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki kwa watejawao na maendeleo ya teknolojia yanayoendelea kutokeaduniani.