Burudani

Bill Nas na Mr T Touch waungana tena kwa ngoma mpya itakayotoka mwezi huu

Mkali wa ‘Chafu Pozi’ Bill Nas amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula ambapo ameahidi kuachia wimbo kabla mwezi huu (January) haujaisha.

Bill Nas ni miongoni kati ya wasanii waliofanya vizuri kwa mwaka jana na kupitia kipindi cha Zero Planet ya Ice Fm amesema, “Plan zangu nyingi tu mtaona matunda yake soon natoa wimbo mpya.”

Alipoulizwa kuhusu soon ikiwa ni mwezi gani Nas amesema “mwezi huu wa kwanza” na mpishi wa ngoma hiyo ni Mr T Touch yule yule aliyefanya Chafu pozi

Kuhusu ile kauli ya real hip hop aliyoisema Young Killer ameirudisha kupitia wimbo wake Na, s amesema “ni kukua kwa muziki, hata program zimebadilika za kugonga muziki kwahiyo hatuwezi kubaki pale pale.”

Hata hivyo hajataja wimbo unaitwaje, ni collabo au kafanya peke yake ila kikubwa amewaomba mashabiki wajiandae kumsapoti katika karata yake nyingine

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents