Burudani

Bin Laden wa Tongwe aeleza alivyopoteza baada ya kutekwa

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tongwe Records, Bello Bin Laden amefunguka kueleza vitu vyake vilivyopotea baada kutekwa na watu wasiojulikana mwezi April mwaka huu.

Akiongea katika kipindi cha Flavour Express cha Maisha FM ya Dodoma, Bin Laden amesema, amepoteza project za wasanii kibao akiwemo Bill Nas, Belle 9 na wengine.

“Kuna project zangu zimepotea studio, project ya Bill Nas, project ya Kamikaze, Belle 9, project ya Stamina kibao zimepotea studio,” amesema Bin Laden.

Bin Laden ameongeza kuwa kwa sasa anahasira sana kwenye muziki kwa hiyo watu wasiombe apande gari aje tena Dar es Salaam kwa kuwa kwa sasa bado yupo nyumbani kwao Dodoma kwa mapumziko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents