Habari

China yafunga vivutio vya utalii kuhofia madhara ya makombora ya Korea Kaskazini

China imetangaza kufunga vivutio vyake vya asili vya utalii kwa kuhofia madhara makubwa yatakayotokea ikiwemo maporomoko ya ardhi na milipuko ya Volcano kutokana na majaribio ya silaha za nyuklia yanayotekelezwa na Korea Kaskazini.

Milima ya Changbaishan.

Maeneo ambayo serikali ya China imeshatangaza kuyafunga kwa matumizi ya umma ni kreta ya Changbaishan, Mlima Paekto ambao una volcano hai na upo mpakani kati ya Korea Kaskazini na China.

Kutokana na usalama wa watalii na kuepusha usumbufu kwao serikali imelazimika kufunga kwa muda vituo vyetu vya utalii vya asili vilivyopo kusini mwa milima ya Changbai“,Imeeleza taarifa rasmi iliyotolewa jana na Serikali kupitia Bodi ya utalii nchini humo .

SOMA ZAIDI – Jaribio la siri la nyuklia nchini Korea Kaskazini laleta tetemeko la ardhi

Kwa upande mwingine rais wa Marekani, Donald Trump ameguswa na vitisho hivyo na kusema kuwa tayari ameshawasiliana na Rais wa Korea Kusini na kujadiliana jinsi ya kuidhibiti Korea Kaskazini kwa kila namna juu ya utengenezaji wa silaha za kinyuklia.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents