Burudani
Collabo ya Donald wa Afrika Kusini na Diamond iliyopangwa kutoka wiki iliyopita yasogezwa mbele
Msanii wa Afrika Kusini, Donald aliyemshirikisha Diamond kwenye collabo waliyoipa jina la kiswahili ‘Wangu’, amewaomba radhi mashabiki waliokuwa wakitarajia video na audio ya wimbo huo ambao awali ulipangwa kutoka Ijumaa iliyopita 17/07/2015.
Donald aliandika Instagram kuwa watatoa taarifa ya lini video hiyo itatoka.
“Announcement: Apologies to all the fans. Due to some unforseen circumstances theres been a slight delay on the release of the “Wangu” video with my brother @diamondplatnumz We will update everyone soon. THANK YOU FOR YOUR UNDERSTANDING. WE LOVE YOU GUYS”- donaldindenial
Video hiyo imeongozwa na Justin Campos wa Gorilla Films ya Afrika Kusini, aliyefanya video ya ‘Nusu Nusu’ ya Joh makini na ‘No Body But Me’ ya Vanessa Mdee.