MichezoUncategorized

EFL Cup: Man United macho kodo, Chelsea mbele kwa mbele

Usiku wa kuamkia leo umekuwa mbaya kwa klabu ya Manchester United baada ya kutupwa nje ya mashindano ya kombe la EPL na Bristol City katika hatua ya robo fainali.

United ambao wanashika nafasi ya pili katika ligi kuu ya Uingereza, wamepokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza.

Mabao ya Bristol yamefungwa na Bryan katika dakika ya 51 na Smith dakika ya 90 wakati bao la kufutia machozi la United limefungwa na Zlatan Ibrahimovic katika dakika ya 58.

Katika mchezo mwingine wa robo faiali ambao ulichezwa usiku huo Chelsea wamefanikiwa kusonga mbele baada ya kuifunga Bournemouth kwa mabao 2-1.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Willian dakika ya 12 na Morata dakika ya 90 na bao wa Bouurnemouth limefungwa na Dan Gosling katika dakika ya 90.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents