Mitindo

Fashion for Education

Image
Image
Mbunifu wa Mitindo, Ally Rehmtullah akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni ya Kuchangia Mfuko wa Elimu wa Wilaya ya Kisarawe.
Wa kwanza kulia ni Prof. Emmanuel Bavu ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati
ya maandalizi ya Harambee Kisarawe, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya
ya Kisarawe Bi. Khanifa Karamagi pamoja na Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza.

Image
Mwaka 2008 Wialaya
ya Kisarawe ilikuwa na Shule za kata 11, ikilinganishwa na shule 6
zilizokuwapo mwaka 2006. Hata hivyo pamoja na ongezeko hilo shule 11
zilidhihirika kuwa na mapungufu kama ifuatavyo:-
1. Uhaba wa madarasa.
2. Uhaba wa nyumba za walimu na chache zilizopo kutokufikia viwango stahiki.
3. Kutokuwepo mifumo ya maji na umeme.
4. Shule zote kutokuwa na maabara.
5.
Wanafunzi kutembea umabli mrefu kutoka majumbani kwao au kulazimika
kupanga katika nyumba za jamii inayozunguka shule kwa kuwa hakuna
hosteli mashuleni.
Mapungufu yote
yaliyoorodheshwa pamoja na mengine yalithibitika kurudisha nyuma juhudi
za kuimarisha elimu na maendeleo ya wilaya kwa ujumla.
Ili
kuepuka hali hiyo, mapema mwaka 2008 uongozi wa wilaya uliona umuhimu
wa kuhakikisha wilaya inazindua na kubuni mpango mkakati wa
kushirikisha wilaya inazinduka na kubuni mpango mkakati wa kushirikisha
wananchi wa Kisarawe walio ndani na nje ya wilaya, marafiki na wadau
mbali mbali kuchanga kwa hali na mali ili kuboresha miundo mbinu katika
shule zote za kata na kujenga chuo kimoja cha ufundi.
Mpaka sasa jumla ya michango yote ni Tsh. 29, 285,200/= ahadi ni Tsh.
25, 174,500/= na USD 50,000/= pamoja na eneo la ekari 98 kwa ajili ya
ujenzi wa chuo cha ufundi lililotolewa na mwananchi mmoja wa Wiraya ya
Kisarawe.
Kwa wale wateja wa
mtandao wa Zain jinsi ya kuchangia ‘Unatuma ujumbe mfupi wenye neno
ELIMU kwenda namba 15620 ambapo kampeni hii itaanza rasmi 1st March
2010 na kila SMS utakayotuma utakatwa shilingi 250/=. Pia kwa wale
wanaotumia huduma ya ZAP wanaweza kuchangia kwa kutumia hiyo namba ila
kima cha chini ni shilingi 1000/=

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents