Habari

Imeelezwa Saudia Arabia imemtuma mwendesha mashtaka wao mkuu kwenda kukutana na maafisa wa ujasusi wa Uturuki kuongelea suala la Khashoggi

Imeelezwa Saudia Arabia imemtuma mwendesha mashtaka wao mkuu kwenda kukutana na maafisa wa ujasusi wa Uturuki kuongelea suala la Khashoggi

Imeelezwa kuwa Mwendesha mashitaka mkuu katika taifa la Saudi Arabia jana usiku alikutana na maafisa wa shirika la ujasusi la Uturuki kama sehemu ya uchunguzi wa mauaji ya mwandishi habari na mkosoaji wa serikali ya Saudi Arabia Jamal Khashoggi.

Kwa wa mujibu wa DW, Shirika la habari la kibinafsi la DHA limeripoti kuwa Mwanasheria mkuu huyo Sheikh Saud al-Mojeb, aliyekwenda mjini Istabul wiki hii, aliondoka hotelini mwake usiku jana akisindikizwa na msafara na kwenda katika ofisi za kikanda za shirika la Ujasusi la Uturuki. Hakukuwa na taarifa yoyote kuhusu kilichojadiliwa.

Khashoggi aliyekuwa na umri wa miaka 59, mchangiaji wa gazeti la Marekani la WASHINGTON POST, aliuawa baada ya kuingia katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul Oktoba 2 kuchukua nyaraka za kufunga ndoa na mchumba wake wa Kituruki. Mwili wake haujapatikana mpaka sasa.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents