Burudani
Ja Rule kufungwa miaka miwili
Rapper MC maarufu kama Ja Rule aliyewahi kuwa na bifu kubwa na 50 Cent amejikuta akikwaruzana na sheria huko kwao Marekani na kupewa hukumu ya miaka miwili jela.
Rule alipewa sentensi hiyo na jaji kufuatia kukamatwa na bunduki iliyokuwa na shaba katika gari lake. Mashitaka hayo yamewashangaza wengi kwani yamefanana na yale ya rapper Lil Wayne yaliyompelekea kufungwa mapema mwaka jana kwa muda wa miezi nane,
Wadau wengi wa muziki wa Ja rule pamoja na mashabiki wake wamehoji kisa ch rule kufungwa miaka miwili kuliko miezi nane kama ya Wayne lakini Serikali ya huko Mreakni hawajatoa tamko mpaka sasa.
Ja amesema tatadondosha albam kabla ya kifungo chake kinachoanza Juni mwaka huu na kuwasihi mafans wakae mkao wa kula.