Siasa

JPM: Nchi yetu ni miongoni mwa nchi 10 zenye maendeleo ya juu, Afrika nafasi ya 6 na duniani ya 52 (+Video)

“Nchi yetu ni miongoni mwa nchi 10 zenye maendeleo ya juu Afrika, katika ripoti ya mwaka 2020 Nchi yetu ya Tanzania inaongoza kuwa mahali penye amani kwa Afrika Mashariki na katika Afrika nzima sisi ni wa 6 na katika Dunia nzima sisi ni wa 52”

 

“Sasa hivi Makao Makuu ya Nchi yetu yapo Dodoma na mimi mwenyewe ninakaa Dodoma, sitashindwa kufanya maendeleo katika Wilaya ya Bahi kwa sababu Bahi na Dodoma ni pua na mdomo,nawahakikishia sitawaangusha, tumetoka mbali”

“Kwenye miaka 5 tutaendeleza jitihada kwa kukamilisha pale tulipoishia, tutaendelea na ujenzi wa vituo vingine vya afya, tutaendelea kuboresha elimu bila malipo, tutahakikisha tunafikisha umeme kwenye Vijiji 16 vilivyobaki kwenye Wilaya hii ya Bahi”

“Tumejenga Hospitali ya Wilaya ambayo ujenzi wake umefikia 95% kwa Tsh Bilioni 1.8, nataka hii Hospitali ya Wilaya imalizike haraka ili wananchi wa Bahi wawe wanatibiwa hapahapa na ndiyo maana ninawaomba mnipe kura nikamalizie kiporo kilichobaki”

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents