Habari

Kampeni ya One Billion Rising kufanyika Feb 14 Coco Beach

Tarehe 14, Februari, 2015, saa 8 mchana, Dar es Salaam itajiunga na wanaharakati duniani kote pale Coco Beach Masaki jijini Dar es Salaam kwa ajili ya One Billion Rising – harakati za wahamasishaji kimataifa kukomesha ukatili dhidi ya wanawake na wasichana.

unnamed

One Billion Rising ilianza kama wito wa kuchukua hatua kutokana na takwimu ya kushtua kwamba mwanamke 1 kati ya 3 duniani atapigwa au kubakwa wakati wa uhai wake.

Kwa kuwa idadi ya watu duniani imefikia bilioni 7, hii inamaanisha zaidi ya wanawake na wasichana bilioni moja.

“Kutakuwa na muziki na kucheza, hivyo tunawaalika Wanaharakati, waandishi, wanafalsafa, watu mashuhuri, wanawake na wanaume kuja kujumuika nasi na kuamka na kuinuka pamoja kukemea ukatili dhidi ya wanawake,” yanasema maelezo.

Ili kufahamu zaidi kuhusu One Billion Rising, tembelea tovuti www.onebillionrising.org au tembelea ukurasa wa Facebook

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents