Michezo
Lewandowski ajitia pingu Bayern Munich
Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski hatimaye amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea timu hiyo mpaka mwaka 2021.
Robert Lewandowski akisaini mkataba mpya
Kupitia mtandao wa Twitter, mshambuliaji huyo ameandika “This club gives me all i need to make my dreams come true! New challenges ahead of us! MiaSanMia! @FCBayern.”
Mshambuliaji huyo raia wa Poland alisajiliwa na timu hiyo mwaka 2014 akitokea Borussia Dortmund zote za ligi kuu ya Ujerumani. Mpaka sasa Lewandowski ameshaifungia Bayern magoli 58 kati ya mechi 77 alizocheza.