Burudani

Mapacha wazungumzia maisha baada ya kupatana na Clouds FM

Rappers wa kundi la Mapacha, wamesema kwa sasa wameamua kufanya kazi na wana amani moyoni baada ya kusuluhisha ugomvi wao na Clouds FM na kutoa ngoma zao mbili.

IMG_5081
Mapacha

Akiongea na Bongo5 member wa kundi hilo, Dotto aka D wa Maunjanja Saplayaz, alisema wao na Vinega bado wana uhusiano mzuri.

“Unajua kuna wengine ni ndugu pale unajua hizi na itikadi tu zimebadilika lakini tunasalimiana kama kawaida. Unajua tunafanya mambo kwa manufaa ya maisha yetu. Tokea tumemaliza tofauti zetu na uongozi wa Clouds Media Group tumepata changamoto hasa kwa wale mashabiki wachache wasiopenda maendeleo na wasioelewa. Unajua kuna watu wengine wanapenda kuona nyie mpo kwenye matatizo kila siku inapotokea mmepata afadhali unakuta hapendi anataka kuona mnataabika tu kila siku. Sasa hivi tunafurahi kwakweli maana tunapa show kama hii ya Fiesta. Unajua unapo kuwa msanii show ni muhimu sana na unapopata show ndo mambo mengine yanaenda.”

Kwa upande mwingine Mapacha wamesema hiphop bado ni muziki unaopendwa zaidi.

“Unajua hiphop ndo muziki ambao umekuwa ukifanya vizuri siku zote hata kwenye show ndo muziki ambao umekuwa una amsha amsha. Hii miziki mingine inakuja na kuondoka lakini hiphop yenyewe ipo palepale. Angalia hata wasanii wengi wanaokuja bongo kwenye show ni wa hiphop. Kwaihyo inaonyesha kabisa hiphop ndo muziki unaofanya vizuri. Na sasa tuna mpango wa kufanya video ngoma zetu hizi mbili maana tunajua tuna deni kwa mashabiki wetu. Kwahiyo wasijali video zinakuja muda si mrefu.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents