Burudani

Mwanamuziki nguli wa Canada Leonard Cohen afariki dunia

Mwanamuziki mkongwe wa nchini Canada aliyekuwa kuwa na uwezo wa kuimba nyimbo za tamaduni mbalimbali, Leonard Norman Cohen amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 82 – kwa mujibu wa taarifa zilizotoka kwenye vyombo vya habari vya nchi hiyo huku chanzo cha kifo cha hakijawekwa wazi.

0f4e9e7f-f4f7-4565-adde-2190b1f1cf06

Muimbaji huyo aliwahi kuwa mwandishi wa riwaya mbalimbali kabla ya kuingia kwenye fani ya uimbaji ambayo ilimttambulisha zaidi duniani kutokana na nyimbo zake kadhaa alizowahi kuziachia ikiwemo “Suzanne”, “I’m Your Man”, “Hallelujah” na nyingine.

Mwaka 2008 Cohen alifanikiwa kujumuishwa kwenye orodha ya wanamuziki mashuhuri wanaoimba muziki wa Rock and Roll kwenye Rock and Roll Hall of Fame. “This is a very unlikely occasion for me. It is not a distinction that I coveted or even dared dream about,” alisema muimbaji huyo baada ya kuingia kwenye orodha hiyo.

Kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 Leonard alipumzika kuimba na kuamua kwenda kuishi katika kituo cha Zen cha Mount Baldy kilichopo Los Angeles lakini baadaye alirudi kwenye kazi yake hiyo.

Mpaka anafariki muimbaji huyo amefanikiwa kuachia albamu 14 huku ya mwisho akiwa ikiwa ni “You Want It Darker” aliyoiachia mwezi uliopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents