Habari

Mwandishi aliyepotea miezi miwili kichwa na miguu yake vyapatikana ufukweni

Kichwa na miguu ya mwandishi wa habari wa Sweden, Kim Wall vimepatikana ufukweni, baada ya mwili wa mwandishi huyo kupotea miezi miwili iliyopita akiwa kwenye ziara ya kikazi na baharia raia wa Denmark.

Kim Wall

Bi. Wall (30) alipotea tarehe 10 Agosti mwaka huu wakiwa kwenye manuari na raia huyo wa Denmark aliyetambulika kwa jina la Peter Madsen.

Kichwa na miguu ya Bi. Wall imeokotwa na waogeleaji katika fukwe za Koge mjini  Copenhagen, Denmark ijumaa ya wiki hii vikiwa vimefungwa na mabegi .

Polisi mjini Copenhagen wamethibitisha kupatikana kwa kichwa na miguu ya mwandishi huyo wa habari ambapo wameeleza kuwa kwenye mabegi kulikuwa visu na vyuma vizito vilivyompelekea kuzama chini ya bahari.

Mkutano wa polisi na waandishi wa habari uliofanyika jana (Jumamosi) kuhusu tukio hilo kwa lugha ya Kidenishi.

Hata hivyo Bwana Peter Madsen (46) amekamatwa na polisi kwa mahojiano tangia tukio hilo lilipotiwe na vyombo vya habari nchini Sweden.

Polisi imesema kwenye mahojiano na mtuhumiwa huyo amekana kumuua huku akidai aliingia kwenye nchini kufanya uchunguzi kwa bahati mbaya akafa ndipo akachukua uamuzi wa kumtupa baharini.

Peter Madsen

Awali taarifa kutoka Associated Press zilieleza kuwa mwanadada huyo huenda alibondwa na vitu vizito akiwa kwenye manuari lakini tayari polisi wamekanusha taarifa hizo kwa kusema fuvu la kichwa cha Bi. Wall halikuwa na hitilafu wala dalili za kupigwa na kitu kizito.

Manuari aliyopanda marehemu Wall aina ya UC3 Nautilus.

Bi. Wall alipanda manuari hiyo ya Denmark akitokea Sweden akiwa na Baharia Madsen ambapo alikuwa akifanya habari za uchunguzi kama mwandishi wa habari.

Wall alikuwa ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea na amewahi kufanya kazi na magazeti makubwa duniani kama The New York Times, The Guardian na Foreign Policy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents