Habari

Naibu Meya wa Arusha ajiuzulu

micheal_kivuyo2

Siku chache baada ya mchafuko kati ya wanachama na viongozi wa CHADEMA na jeshi la polisi, naibu meya wa Arusha amejiuzulu kwa kile kinachosemekana ni ubatili wa matokeo ya kura yaliyofanyika mjini hapo Desemba 18, mwezi uliopita.

 

Micheal Kivuyo aliyepewa nadhifa hiyo kupitia chama cha cha TLP, Tanzania Labour Party ameeleza sababu ya kujiuzulu ni kufuatia kuungana na wananchi wenzake wakazi wa Arusha, kupinga kitendo cha polisi kuwapiga raia na kusababisha mchafuko wa amani ambapo hatimaye watu sita walipoteza maisha yao.

Kivuyo ameitaka serikali kurudia uchaguzi huo ambao unasemekana kuwa wenye utata.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents