Burudani

Nick wa 2 aunga mkono wasanii kuingia kwenye siasa, adai wanaiongezea mvuto

Rapper wa Weusi, na msomi wa Masters, Nick wa Pili amedai amefurahishwa kuona wasanii wakiingia kwenye siasa na kusema kuwa wanaongeza mvuto kwakuwa ni watu wanaoangaliwa na watu wengi.

Dr Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Nick wa Pili
Dr Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Nick wa Pili

Akizungumza na Bongo5 leo, Nick amesema msanii kuingia kwenye siasa na kugombea wadhifa ni haki yake ya msingi katika katiba na wanaweza kuwa na faida kubwa sana ilimradi wawe na vigezo.

“Kwanza msanii kuingia kwenye siasa,kugombea ama kufanya shughuli za kisiasa ni haki yake ya kikatiba inamruhusu na pili msanii anapoingia kwenye siasa inaweza kuwa na faida, anaiongezea siasa mvuto kwasababu msanii anapofanya kitu watu wengi wanaweza kutazama na kumsikiliza,” amesema Nick.

“Kwahiyo msanii anapoingia kwenye siasa ataiongezea siasa mvuto.Siasa ndio kama engine, ndio kitu ambacho kina drive maisha yetu ya kila siku. Kwahiyo kama wasanii wanaingia kwenye engine ni sawa, cha msingi tu kama msanii anataka kugombania uongozi awe na uwezo wa kuongoza,awe na busara, awe na maarifa halafu awe committed, yaani awe amejipanga kufanya uongozi kwaajili ya watu asiingie kwenye uongozi kwaajili ya ajira,” ameongeza rapper huyo wa Nje ya Box.

“Siasa za Tanzania ni rahisi kuingia kwasababu falsafa ni kuchukua form tu,kwamba mimi leo naamka nasema nachukua form kugombania ubunge. Lakini siasa katika nchi ambazo zimekomaa chama ni taasisi ili mfano mpaka ufike nafasi ya kugombea ubunge au wadhifa fulani inabidi uwepo kwenye chama muda mrefu, inabidi ufanye mambo moja ,mbili,tatu yaani kwamfano Marekani hauwezi kuwa rais kama hujawai kuwa member of congress haujawahi kuongoza kwenye congress.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents