Bongo Movie

Picha: Bongo Movie Unit waipa msaada hospitali ya Mwananyamala Dar

Bongo Movie Unit leo wametembelea katika wodi ya akinamama na watoto katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam na kutoa msaada wa vitu wenye thamani ya shilingi milioni 15 kama njia ya kuishukuru jamii kwa mafanikio yao.

Steve na JB wakiwa na akinamama yenye watoto wodini
Steve na JB wakiwa na akinamama yenye watoto wodini

Mwenyekiti wa Bongo Movie Unit,Steve Nyerere amesema wameamua kufanya hivyo ili kurudisha walichokivuna kwa jamii.

“Tunaamini tunapata kipato kikubwa kutokana na filamu zetu na wateja wetu wa kuu ni akinamama,” Steve ameiambia Bongo5. “Kwahiyo tukaona tunatakiwa wakati tunatimiza miaka mitatu tangu bongo movie ianzishwe, tuwatembelee akinamama katika ma hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam na kutoa misaada, ndio tukaanza na hospitali ya MwananyaMAla,tukatoa misaada ya vitu mbalimbi kama nguo za watoto,mabeseni, yaani tumeangalia mahitaji yao kwa ujumla. Kwahiyo leo tumetoa msaada wa vitu vyenye thamani ya kama milioni 15.”

JB akiwa amekaa na mama mwenye mtoto wodini
JB akiwa amekaa na mama mwenye mtoto wodini

Wasanii wakiwa wamebeba baadhi ya vitu
Wasanii wakiwa wamebeba baadhi ya vitu

IMG-20140326-WA0009

IMG-20140326-WA0023

IMG-20140326-WA0025

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents