Burudani

Picha: Davido akutana na rapper na mchumba wa zamani wa Ciara, Future

Davido amepost picha Instagram aki hang pamoja na rapper wa Marekani ambaye pia ni baba wa mtoto wa muimbaji Ciara, Future.

Davido and Future-1
Davido akisalimiana na Future Hendrix

Ukaribu baina ya wasanii wa Nigeria na mastaa mbalimbali wa ‘unyamwezini’ ni ishara kwamba muziki wa Afrika unaendelea kupenya taratibu Marekani, japo kwa kupitia wasanii wa Nigeria zaidi.

Davido and Future-2

Wiki hii pia tumeshuhudia Alicia Keys na mumewe Swizz Beatz wakithibitisha kuwa ni mashabiki wakubwa wa Wizkid, kwa kupost video Instagram wakicheza nyimbo zake.

Timaya n Riri
Timaya na Rihanna

Siku chache zilizopita Rihanna naye alionekana akicheza wimbo wa msanii wa Nigeria, Timaya ambaye pia walipiga picha pamoja huko Barbados katika tamasha la Cropover.

Drake naye aliamua kufanya remix ya ‘Ojuelegba’ ya Wizkid baada ya kuupenda mwenyewe.

Hii yote ni tafsiri kwamba muziki wa Afrika kwa ujumla umeanza kuwaingia mastaa mbalimbali wa nje, na itasaidia kuutambulisha muziki wa Afrika kwa ujumla hata kama ni kwa kupitia wasanii wa Nigeria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents