Habari

Polisi yawasaka wauaji wa Rais nchini Haiti

Jeshi la Polisi nchini Haiti, linawasaka washukiwa waliohusika na mauaji ya Rais wa nchi hiyo Jovenel Moise katika kipindi hiki ambacho nchi hiyo ipo Chini ya sheria za Kijeshi.

Vikosi vya Usalama vimekabiliana vikali na washukiwa wa tukio hilo katika Mji Mkuu Port-au-Prince baada ya shambulizi la usiku wa manane kwenye makazi binafsi ya Rais.

Mkuu wa Polisi ,Leon Charles amesema Polisi nchini Haiti imewauwa washukiwa wanne na wawili wamekamatwa huku washukiwa wengine wa kikundi hicho wakiingia mafichoni.

Mamlaka za kiusalama nchini humo,bado hazijatoa taarifa za kina kueleza hasa nia ya wauaji kutekeleza mauaji ya Rais huyo.

Mke wa Moise ,Bibi Martine alijeruhiwa na anaendelea kupokea matibabu mjini Miami nchini Marekani.
Nchi ya Haiti imetangaza wiki mbili za maombolezo ya aliekua kiongozi Mkuu wa nchi na Waziri Mkuu Claude Joseph ametangaza sheria za kijeshi na kusema amekaimu uongozi wa nchi hiyo kwa sasa.

By-BAKARI WAZIRI

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents