Burudani

R.Kelly atangaza kutoa album ya muziki wa ‘House’

Muimbaji wa R&B, Robert Kelly ametangaza kuwa anatarajia kutoa album ya muziki wa ‘House’ ambayo tayari ameanza kuiandaa.

r

“I’m working on a house album right now and I want y’all to know, it’s coming,” Alisema Kelly.

R.Kelly ambaye album yake ya 12 ‘Black Panties’ iliyotoka december 10, 2013 Marekani, imekamata nafasi ya 4 katika Billboard 200 huku ikiwa imeuza nakala 133,000 kwa mujibu wa Nielsen SoundScan, aliongeza:

“Najisikia nina uwezo wa kufanya kitu chochote kwenye muziki kwasababu mimi mwenyewe ni muziki, kama nyinyi wote”.

Wakati anatoa ahadi ya album ya miondoko ya ‘House’, Kelly pia mwezi March mwaka huu alisema anatarajia kutoa album nyingine mwaka huu ‘White Panties’ ikiwa ni mwendelezo wa album ya mwaka jana ‘Black Panties’.

https://www.youtube.com/watch?v=Y-YftkPPEvU

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents