Burudani

Shaa asema hapendi tabia ya mashabiki kumshindanisha na Vanessa Mdee

Muimbaji wa ‘Sugua Gaga’ Sarah Kaisi a.k.a Shaa ameeleza jinsi anavyokerwa na tabia ya baadhi ya mashabiki wa muziki wanaojaribu kuwashindanisha kisanii na muimbaji nwenzake Vanessa Mdee.

shaa sugua gaga

Shaa ambaye ameachia wimbo mpya ‘Toba’ wiki iliyopita, amesema si sawa kushindanishwa na Vee Money kwasababu wote wanapeperusha bendera ya Tanzania.

“Niwambie ukweli sipendi sana hii tabia ya watanzania kunishindanisha na Vanessa Mdee au kitendo cha kuwashindanisha wasanii wa nyumbani,” alisema Shaa kupitia Planet Bongo ya EATV. “Huwezi kuwashindanisha watu ambao wapo kwenye boti moja, Mimi Shaa pamoja na Vanessa Mdee wote tunapeperusha bendera moja ya Tanzania hivyo unapotupambanisha ili iwe nini, ni bora hata ungenipambanisha na msanii kama Yemi Alade sababu yule ni msanii kutoka nchi nyingine” alisema Shaa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents