Makala

Super Sunday Makala: Njia tano rahisi kuweza kufikia malengo yako (+video)

Unaambiwa kuwa mpweke haimaanishi kuishi pekee yako, bali kuishi bila malengo ni upweke unaotesa zaidi.

Hivyo ni muhimu kuweka malengo ila kuifanya safari yako hapa ulimwenguni kuwa na unafuu. Hata hivyo kuwa na malengo pekee haitoshi bali kunahitajika mikakati ili kufanikisha kile ulichodhamiria.

Hivyo basi, Joel Nanauka ambaye ni mwandishi wa vitabu na mwalimu katika masuala ya mafanikio anaeleza kanuni tano muhimu zitakazokuwezesha kufikia malengo yako kwa urahisi zaidi.

Hapa chini nimeandika yale yote aliyozungumza katika mahojiano aliyofanya na Bongo5.

1. Gundua Kusudi Lako

Kila mtu aliyekuja duniani ameumbwa kwa sababu maalum na kama hujafahamu kusudi lilokufanya uje duniani hatoweza kufanikiwa kama inavyotakiwa.

Ni sawa na kusema samaki anaweza kuogelea kwa sababu ameumbwa kukaa majini. Sasa na wewe kuna mahali unatakiwa uishi na ufanye hayo, watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwa sababu wapo sehemu ambazo sio sahihi.

Sehemu ambayo umeumbwa kuifanya hautumii nguvu kubwa kupata matokeo, yaani unakuwa umejengewa uwezo wa kufanya kwa ufanisi kuliko kawaida.

2. Wekeza na Jenga Uwezo

Kuwekeza na kujenga uwezo katika lile ambalo umekusudia, unapoanza kugundua kusudi lako na kuanza kuliishi ni safari ya muda mrefu sana, kwa hiyo ni lazima uhakikishe kila wakati unajenga uwezo wako.

Mwanauchumi maarufu nchini Italy, Vilfredo Pareto alikuja na kitu kinaitwa 80, 20 Rule. Maana yake unapogundua sehemu ambayo unatakiwa kuishi kila siku hakikisha asilimia 80 ya muda wako, rasilimali na kila ulichonacho vinalenga kujenga uwezo katika kile ulichonacho.

3. Jenga Mtandao

Hakikisha unajenga mtandao wa watu ambao watakupeleka kwenye kila ambacho unataka kukifanya.

Jeff Olson kwenye kitabu chake cha The Slight Edge, anasema kila mmoja wetu sisi ni wastani wa watu watano wanaotuzunguka, kwa maana nyingine wale wanaokuzunguka wanaweza kukufanya ufanikiwa au usifanikiwe.

Kwa hiyo fanya ukaguzi wa marafiki ulionao, wale wanaokurudisha nyuma, kukukatisha tamaa, wanaokuondoa kwenye mstari jaribu kuwaondoa. Pia kuna marafiki itabidi uwatafute na kuna ambao itabidi uongeze muda wa kukaa nao, kama unataka kufanya biashara tafuta wanaofanya biashara.

Your network is your networth, thamani yako tunaweza tukaipima katika marafiki ambao wanakuzunguka.

4. Kujiamini

Watu wengi sana wana ndoto, wengi wemejenga mtandao, wamejitahidi kujua ni eneo gani wameitiwa lakini hawana ujasiri kwa sababu wameambiwa mara nyingi sana hawataweza.

Utafiti mmoja unaeleza kuwa mtoto mdogo anapokuwa amezaliwa hadi kufikisha umri wa miaka mitano, huwa anakuwa ameambiwa neno hapana mara 40,000 lakini anakuwa ameambia neno ndiyo mara 5,000 tu.

Hii maana yake nini?, kuna watu wengi ambo wanaotuzunguka hawaamini katika uwezo wetu, inawekena ni wazazi, waalimu, mabosi, marafiki nakadhalika.

Kama watu milioni moja watakuambia unaweza lakini wewe ukaamini hauwezi, basi hautaweza, na kama watu hao wakakuambia hauwezi lakini wewe mwenyewe ukaamini unaweza basi utafanikiwa. Hivyo nguvu ya kutekeleza na kufikia kilele cha ndoto yako ipo mikoni mwako.

5. Chukua Hatua

Watu wengi sana wana ndoto, malengo na mambo wanayotaka kufanya lakini hawachukui hatua ya kuanza kutekeleza yale ambayo yamekusudiwa.

Mwandishi maarufu Marekani, Mark Twain alisema miaka 20 kuanzia leo utajutia zaidi kwa mambo ambayo hukuyafanya kuliko yale ambayo uliyafanya.

Mwanasaikolojia mmoja alitoa msemo uitwao; 18, 40, 60. Maana yake ni ukiwa na miaka 18 haufanyi vitu kwa sababu kila wakati unajiuliza watu wanasemaje, watanionaje, watanichukuliaje na ukifikisha miaka 40 unagundua hakuna mtu aliyekuwa anakuwazia.

Ukifisha miaka 60 unagundua kati ya watu wote hakuna aliyekuwa anakuwazia. Maana yake ni kwamba watu wengi wanajutia kwa sababu wanataka kuwapendezeshe watu, hapana!, live your life, live your dream.

Watu wengi ukiwaambia chukua hatua wanasema sina mtaji, hapana!, kanuni ya mafanikio inasema; anza na ulichonacho pale ulipo kwa namna unavyoweza, usisubiri uwe na vingi ili uwe kuanza. Kwenye kila mbegu kuna mti, kwenye kila mti kuna matunda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents