Michezo

Tyson: Nimekuwa nikitumia Cocaine ili kukabiliana na ugonjwa wa kiakili

Bingwa wa ngumi uzani mzito duniani Tyson Fury kutoka nchini Uingereza, amesema amekuwa akitumia Cocaine ili kumsaidia kukubiliana na matatizo ya kiakili.

390f5ada00000578-0-tyson_fury_has_admitted_taking_lots_of_cocaine_and_claimed_he_ho-a-1_1475658779309

Bondia huyo kutoka Uingereza amesema kuwa amekuwa akiugua ugonjwa wa kiakili kwa miaka kadhaa na hajafanya mazoezi tangu mwezi Mei.

“Nimekuwa nje nikilewa ,Jumatatu hadi Ijumaa hadi Jumapili na kutumia Cocaine,”Fury aliambia jarida la Rolling Stones.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni siku mbili baada ya Fury kudai katika mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu,kabla kukana madai hayo saa tatu baadaye akisema alikuwa akifanya utani.

Akiongea masuala ya kuhusu afya yake ,Fury aliongezea: Siwezi kukabiliana na matatizo haya na kitu kinachonisaidia ni wakati ninapokunywa ili nitoe matatizo hayo akilini, wanasema nina ugonjwa wa kiakili.Nahisi huzuni.Niingependa mtu aniue kabla sijajiua.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents