Habari

Video: Serikali yaweka mkakati wa Wanawake kumiliki ardhi

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema katika nchi ya Tanzania wanawake na wanaume wana haki sawa ya kutumia na kumiliki ardhi .

Naibu Mabula ameyazungumza hayo, leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Salma Mohamed Mwasa, lililohoji

Je? Serikali ina mkakati gani wa kuwawezesha wanawake wengi zaidi kumiliki ardhi?

“Katika nchi yetu wanawake na wanaume wana haki sawa ya kutumia ardhi misingi hii imewekwa katika ibara ya 54 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo inatoa haki ya kikatiba ya kumiliki mali kwa kila mtu pasipo kujali jinsi,” alisema Mabula.

“Kwa upande mwingine kifungu namba 4 pointi 2 pointi 4 kifungu kidogo cha kwanza cha sera ya Taifa ya ardhi 1995 na kifungu cha 3 sehemu ndogo ya 2 ya sheria ya ardhi sura namba 13 na sheria ya ardhi ya vijiji sura namba 114 zinaelekeza kuwa haki ya kila mwanamke kupata, kumiliki, kutumia na kufanya miamala inayohusu inayohusiana na ardhi itakuwa sawa na haki ya mwanaume kwa kiwango na masharti yaleyale,” aliongeza.

“Pamoja na kuwepo kwa matamko ya kikatiba na Kisheria yanayolinda haki ya wanawake kumiliki ardhi bado kuna changamoto hususani katika maeneo ya vijiji ambapo wanawake wengi wananyimwa haki kumiliki ardhi kutokana na mila, desturi na kaiba za baadhi ya makabila zinazowabagua wanawake kwa kugawa ardhi kwa viongozi wa familia ambao kwa kawaida ni wanaume na kuwanyima wanawake haki ya kurithi mali ya familia.”

“Jitihada za kuondoa mila na desturi hazitafanikiwa kutokana na kushindwa katika utekelezaji kutokana na mfumo dume na uelewa mdogo wa umma kuhusu sera na sheria zilizopo. Katika kukabiliana na changamoto hii wizara yangu inafanya juhudi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho katika sera ya taifa ya ardhi ambayo kwa kiasi kikubwa imeweza kuwashirikisha wanawake ili wafahamu haki yao ya kupata ardhi bila vikwazo vinavyotoka na mila desturi bila vikwazo.”

Video:

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents