Burudani
Video/Picha: Wanafunzi wa chekechea wa Aghakan wamwalika Ommy Dimpoz
Muziki wa Ommy Dimpoz umefanikiwa kuwateka pia watoto wadogo kiasi ambacho kiliwafanya watoto wa chekechea wa shule ya awali ya Aghakan kumwalika Ommy Dimpoz wiki hii shuleni hapo na kufurahi pamoja nao.
“Nilipata mualiko wa shule ya awali ya Aghakan kuwa watoto wanapenda sana nyimbo zangu so nikawatembelea coz waliomba mwalimu wao wanataka kuniona aisee ilikuwa balaa sana maana tupogo mpaka watoto wa kidosi,” Ommy ameiambia Bongo5.
Mambo mengine aliyofanya ni pamoja na kusaini autograph kwa watoto hao.