Burudani

Wasafi TV & Radio havipo kushindana na chombo chochote – Diamond

Msanii Diamond Platnumz amesema Wasafi FM na TV si kwa ajili ya mashindano na vyombo vingine vya habari.

Akizungumza visiwani Zanzibar Diamond amesema vyombo hivyo ni kwa ajili ya kuondoa matabaka miongoni mwa wasanii na kukuuza muziki.

“Ninaomba watu waelewe kabisa hakipo katika kushindana na kitu chochote au kushinda na chombo chochote,” amesema Diamond.

Diamond na timu yake ya Wasafi kwa sasa wapo visiwani Zanzibar kwa ajili ya kusaka vipaji vya utangazaji ambavyo vitapewa nafasi katika vyombo hivyo vya habari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents