Burudani

Chege akanusha kuvaa hirizi kwenye picha iliyozagaa mtandaoni

Chege Chigunda amekanusha vikali tuhuma zilizotokana na kusambaa kwa picha akiwa jukwaani na huku mkononi mwake (karibuni na kwapa) akiwa na kitambaa cheusi ambacho baadhi ya watu wanahisi ni hirizi.

11007849_921713231192706_719149458_n

Mtu wa kwanza kuikuza picha hiyo na kuandika kuwa ana mashaka kuwa kitambaa hicho huenda kikawa hirizi, ni Maimartha Jesse.

“Angalia mkono wa kushoto wa chegge @chegechigunda hiiii ni hirizi ? any way isiwe kesi jiachie chege ila mziki mziki wako naupenda hata ukiniroga saw a Tu…japo cna imani hiyoo,” aliandika mtangazaji huyo wa zamani wa EATV.

AkqbPWJwqIRBi0KzTyRRasTHfc-tP94D4_IKgl5l1gWK

Kauli hiyo ya Maimartha ilimfanya Chege kuamua kutoa ufafanuzi.

“Ushamba+roho mbaya+uandishi bila kusomea ni hatari sana hahaaahahahahahhaa eti waandishi magumashi wanadai nimevaa hirizi hahahhaaaaa hii tulivaa juzi Dodoma siku ambayo alifariki msanii mwenzetu marehemu mez b,msiwe vimbele mbele @maimarthawajesse @waandishimagumashi,” aliandika Chege.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents